The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe heights [Al-Araf] - Swahili translation - Rowad Translation Center - Ayah 150
Surah The heights [Al-Araf] Ayah 206 Location Maccah Number 7
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ [١٥٠]
Na wakati aliporudi Musa kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kuhuzunika, akasema: Ni mabaya mno mliyonifanyia nyuma yangu! Je, mmeiharakisha amri ya Mola wenu Mlezi? Na akazitupa chini mbao zile, na akamkamata kaka yake kichwa akimvuta kwake. (Haarun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika kaumu hawa waliniona kuwa mimi ni dhaifu, na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui zangu, wala usiniweke pamoja na kaumu madhalimu.